Sarufi nimfumo na kanuni za lugha zinazomwezesha mtumiaji wa lugha kuitumia lugha husika kwa usahihi. Mfumo huo humwezesha mzungumzaji kutunga sentensi zisizo na kikomo ambazo hukubalika na wazawa wa lugha wanaoifahamu lugha hiyo barabara. Hivyo ni dhahiri kwamba kila lugha ya mwanadamu huwa na mpangilio na sheria zinazoilinda ili kuifanya kuwa toshelevu na sanifu, na uzingatiwaji wa kanuni na taratibu hizo kwa mtumiaji humfanya na kumtambulisha kama mmilisi wa lugha hiyo.
Sheria za lugha zimegawanyika katika makundi manne yanayojulikana kama matawi ya Sarufi ambayo ni pamoja na; matamshi, maumbo, muundo na maana.
Sarufi matamshi ni tawi la sarufi ambalo limejikita katika kuchunguza sauti na matamshiyanayotumika katika lugha Fulani na kulinda matumizi sahihi ya matamshi hayo baina ya watumiaji wa lugha hiyo. Lugha ya Kiswahili kama zilivyokuwa lugha zote duniani ina matamshi ya aina mbili; Irabu na konsonanti.
A. Irabu
Irabu ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasi na kuwepo kizuizichochote katika mkondo hewa utokao mapafuni ukipitia katika chemba ya kinywana chemba ya pua kwenda nje. Lugha ya Kiswahili inazo Irabu tano ambazo ni; /a/, /e/, /i/, /o/, na /u/.
B. Konsonanti
Konsonanti ni aina ya sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo hewa kutoka mapafuni, ukipitia chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Katika lugha ya Kiswahili zipo jumla ya konsonanti zifuatazo; /b/, /ch/, /d/, /dh/, /f/, /g/, /gh/, /h/, /j/, /k/, /l/, /m/, /n/, /ny/, /ng'/, /p/, /r/, /s/, /sh/, /t/, /th/, /v/, /w/, /y/ na /z/.
Hili ni tawi la sarufi ambalo hujishughulisha na uchunguzi wa maumbo mbalimbali ya maneno katika lugha ya Kiswahili. Maumbo hayo ni; silabi, mofimu na neno lenyewe.
A. Silabi
Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi fungenasilabi huru. Silabi huru ni zile ambazo huishia na irabu.
Ilhali silabi funge ni zile zinazoishia na konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni nadra kuzipata maana lugha hii inatumia silabi huru lakini hupatikana katika maneno ya Kiswahili yanayokopwa kutoka katika lugha nyingine.
B. Mofimu
Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha lugha ambacho kina uwezo wa kusitiri maana ya neno ambalo kwalo limeundwa. AU ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana kisarufi.
Mofimu huru ni aina ya mofimu ambayo huweza kusimama pekee na kujitosheleza kimaana yaani huwa na sifa ya neno. Mfano; mama, Baba, Dada, Kaka, Mjomba, Shangazi n.k. Kwa kuangalia utagundua kuwa mofimu huru haziwezi kugawanyika zaidi na kubeba maana kisarufi, kwa maana kwamba mofimu 'baba' ikigawanywa ba-ba, 'ba' hii haina maana yoyote kisarufi zaidi ya kuwa silabi.
Mofimu tegemezi ni aina ya mofimu ambayo huweza kuvunjwavunjwa na kubeba maana kisarufi, mofimu tegemezi hutegemeana ili kuleta maana kamili ya neno.
Mfano; neno 'anakula' limeundwa na mofimu zifuatazo:- [a-na-kul-a] ambazo kila moja hubeba dhana Fulani ya kisarufi.
Ni mofimu zinazopachikwa nyuma au mbele ya mzizi wa neno ili kubadilisha dhana ya neno. Kwa kuwa mofimu hizo hupachikwa sehemu mbili tofauti, tunapata aina mbili za viambishi kwa mujibu wa nafasi zake katika nenoyaani; viambishi awaliambavyo hupachikwa mwanzoni au nyuma ya mzizi wa neno,viambishi katiambavyo hupachikwa katikati ya neno (Kiswahili hakina viambishi hivi) na viambishi tamatiambavyo hivi hupachikwa mbele au mwishoni mwa mzizi wa neno. Mfano:
VIAMBISHI AWALI | MZIZI WA NENO | VIAMBISHI TAMATI | NENO JIPYA | ||
A | na | chez | ew | a | Anachezewa |
Wa | li | chez | ean | a | Walichezeana |
Tu | ta | chez | e | a | Tutachezea |
NAFSI | UMOJA | UWINGI |
Ya Kwanza | Ni- | Tu- |
Ya Pili | U- | M- |
Ya Tatu | A- | Wa- |
NYAKATI | MOFIMU |
Uliopo | -na- |
Uliopita | -li- |
Ujao | -ta- |
Mzizi | Kiambishi cha Kauli | Kiambishi tamati maana | Neno jipya | Kauli | Viambishi vya kauli |
Chez | a | Cheza | Kutenda | -a | |
e | a | Chezea | Kutendea | -e- | |
Pig | ian | a | Pigiana | Kutendeana | -ian-/-ean- |
iw | a | Pigiwa | Kutendewa | -iw-/ew- | |
Som | esh | a | Somesha | Kutendesha | -ish-/esh- |
eshw | a | Someshwa | Kutendeshwa | -ishw-/eshw- | |
Lim | ik | a | Limika | Kutendeka | -ik-/-ek- |
an | a | Limana | Kutendana | -an- | |
w | a | Limwa | Kutendwa | -w- |
Mzizi wakitenzi ni sehemu ya neno inayobakia mara baada ya kuondoa viambishi vyote vya awali na tamati katika neno hilo. Mfano: - a-na-chez-a {-chez-}, m-ku-lim-a {-lim-}
Mzizi funge ni ule ambao hauwezi kujikamilisha kimaana yaani hauwezi kusimama kama neno. Mfano; -lim-, -chez-, -imb- n.k.
Mzizi huru ni ule ambao huweza kusimama kama neno na ukichanganuliwa zaidi hupoteza maana yake ya msingi. Mfano; Kinu, Kazi, Arifu, Sali n.k.
Shina la kitenzi ni sehemu ya neno ambayo huongezwa viambishi fuatishi (tamati) au nisehemu ya neno ambayo hubakia baada ya kuondolewa viambishi tangulizi. Mfano:- chez+a = cheza, lim+a = lima. Sehemu hii ya neno hutumika kuundia neno jipya. Shina sahili – hili ni shina ambalo huundwa na mofimu moja tu ambayo ni mzizi wa neno hilo, huwa ni mofimu huru, Mfano; Kesho, jana, kitabu, jarida n.k.
Shina changamano – shina hili huundwa na mzizi na kiambishi tamati maana. Mfano; cheka, lala, lia, kula n.k.
Shina ambatani – shina hili huundwa na mofimu mbili ambazo ni huru. Mfano; mwana + kwenda = mwanakwenda, mbwa + mwitu = mbwamwitu
Uambishaji ni ule utaratibu wa kuongeza viambishi katika mzizi wa neno, ili kulipa neno maana ya ziada. AU ni hali ya kubadilishabadilisha mofimu katika mzizi wa neno ili kuonesha upatanisho wa kisarufi katika tungo hiyo.
Kiambishi ni sehemu (mofu) ambayo huambikwa kwenye mzizi wa neno ili kulipa neno hilo maana ya ziada. Tunapopachika viambishi hivyo mwanzoni mwa mzizi wa neno hali hiyo huitwa ‘uambishaji’. Uambishaji upo wa aina mbili; Unyambuaji au unyambulishi: Huu ni aina ya uambishaji unaosababisha neno kubadilika kutoka kategoria moja hadi nyingine. Na Mnyambuliko: Ni aina ya uambishaji ambao huhusisha kurefusha nenona kuliweka katika hali tofauti za katagoria ileile.
Uambishaji wa vitenzi – Uambishaji wa vitenzi hujitokeza kwa kutegemea dhima tofauti tofauti za mofimu kama vile:
Mfano: mzizi –lim- unaweza kupachikwa viambishi hivyo na kuweza kubadilika kidhana kama ifuatavyo:
A-na-lim-a
Hu-lim-a
U-me-lim-a
Ni-na-vyo-lim-a n.k.
Uambishaji wa majina Uambishaji wa majina huwa unazingatia upatanisho wa kisarufi kimofolojia ambao hujikita katika kuangalia alomofu tofauti zinazowakilisha ngeli moja katika umoja na uwingi wa majina hayo.
Kwa mfano:
UMOJA | WINGI | ALOMOFU |
m-tu | wa-tu | M/WA |
m-ti | mi-ti | M/MI |
ki-ti | vi-ti | KI/VI |
u-gonjwa | ma-gonjwa | U/MA |
Ø-fisadi | ma-fisadi | Ø/MA |
Ø-kaka | Ø-kaka | Ø/Ø |
Uambishaji wa vielezi Vielezi katika lugha ya Kiswahili havitokani na kategoria nyingine ya maneno, bali ni maneno ya kawaida yanayopatikana katika lugha na si rahisi kupachika mofimu yoyote katika maneno hayo isipokuwa vielezi vichache ambavyo hupatikana kwa kupachikwa kiambishi awali cha namna {ki-} katika kivumishi au nomino mfano: ki-jinga, ki-janja, ki-toto, ki-raia, ki-puuzi n.k.
Ni hali ya kupachika viambishi tamati katika mzizi wa neno. Mofimu hizo huitwa mofimu fuatishi.
Ukitazama kwa makini utangundua kwamba unyambulishaji mara nyingi hubadilisha neno kutoka katika kategoria moja na kuipeleka katika kategoria nyingine.
Vitenzi vya Kiswahili huwa na tabia tofauti tofauti zinazotokana na dhima za mofimu ambazo hupachikwa katika vitenzi hivyo, hivyo kulingana na dhima za mofimu, vitenzi vya Kiswahili huwa na tabia zifuatazo:
Mfano:
NGELI | KIAMBISHI CHA O- REJESHI | MFANO |
A-WA | -YE- na -O- | Aliyepiga / Waliokuja |
U-I | -O- na -YO- | Uliokatwa / Iliyokatwa |
LI-YA | -LO- na -YO- | Lililochanika / Yaliyochanika |
KI-VI | -CHO- na -VYO- | Kilichovunjika / Vilivyovunjika |
I-ZI | -YO- na -ZO- | Iliyofungwa / Zilizofungwa |
U-ZI | -O- na -ZO- | Uliokatika / Zilizokatika |
U-YA | -O- na -YO- | Ulionipata / Yaliyonipata |
KU | -KO- | Kulikotokea |
PA-MU-KU | PO-MO-KO | Pale alipoingia / Mule alimotokea / Kule alikofunga |
Ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa ambazo huwa na maana (maana yaweza kuwa ni ya kileksika au kisarufi).
Ni aina ya neno ambalo hutaja mtu, kitu, mahali, hali na kitendo. Mfano; Mwajuma, Kalamu, Mwanza, Udakitari, Kulima n.k.
Nomino za pekee: Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si chengine chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima,maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomono za pekee huwa kubwa hata kamanomino hizi zinapatikana katikati ya sentensi. Mfano; baba, Asha, Tanzania, Dodoma, Kilimanjaro, Victoria n.k.
Nomino za jamii: Hizi kwa jina jengine huitwa nomino za jumla. Nomino hizihazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa nimtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Kelvin, Tuafu ama Zawadi.Ikiwani ziwa halitambuliwi kama ni Michigan , Victoria au Nyasa, yaani hutaja vitubila kutaja umahsusi wake kama ilivyo katika nomino za pekee. Hizizinapoandikwa si lazima zianze kwa herufi kubwa isipokuwa zimetumiwamwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vileMkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida,lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee. Mfano wa nomino za kawaida ni; Mwanafunzi, Mwalimu, Mnyama, Mtazamaji, Askari n.k.
Nomino za kawaida: Kundi hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wakuhesabika kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika kwa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine. Nomino ya vitu vinavyohesabika vitanda, nyumba, vikombe vitabu kadahlika. Zile zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maji, mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghlabu nomino hizo huwa sawa katika umoja na wingi.
Nomino za kitenzi jina: Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi . Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino. Mfano; Kulima, Kucheza, Kuimba n.k.
Nomino dhahania: Hizi ni nomino ambazo hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na mwanaadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio vidole na ulimi- yaani vitu ambavyo haviwezi kushikika, kuonekana, na kuonjeka. Mfano; Vita, Njaa, Ugonjwa, Shetani, Mungu n.k.
Ni maneno ambayohutoa ufafanuzi au maelezo ya ziada kuhusu jina ili kuitambulisha vyema.
Vivumishi vya sifa: hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile.Mfano; mzuri, mbaya, mrembo n.k.
Vivumishi vya idadi: vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.Vivumishivya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chakekimetajwa. Mfano; wawili, watano, wengi, wachache n.k.
Vivumishi vya kumiliki: Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu chengine. Mfano;yangu, yake, yako, kwetu n.k.
Vivumishi Vioneshi: Vivumishi vya aina hii huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hiihujengwa na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali. Mfano; hapa, pale n.k.
Vivumishi vya kuuliza: Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu swali “gani? ipi? ngapi?”
Vivumishi vya pekee: Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli yanomino ambayo kinaivumisha. Mizizi vivumishi hivi ni -ote, -o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, -ingineo, -ote. Huonyesha ujumla wa kitu au vitu-o-oteKivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua”– enyeKivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino Fulani. –enyeweKivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani.– ingineKivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu Fulani. – ingineoKivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.
Vivumishi vya A- unganifu: Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hikihuandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwaawali. Vivumishi vya aina hii hutumika kuleta dhanna zifuatazo: -Umilikaji-Nafasi katika orodha. Mfano; wa kwangu, wa Juma, ya tano ya Sita n.k.
Maana ya vielezi: Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi auvielezi vyengine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi , namnagani na hata mara ngapi?
Vielezi vya namna au jinsi. Vielezi vya namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vyanamna vipo vya aina kadhaa.
Vielezi vya idadi. Vielezi vya namna hii huonyesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au kwa kiasifulani. Mfano; amempiga mara mbili.
Vielezi vya mahali. Vielezi vya namna hii huonyesha mahali ambapo kitendo kinatokea.Huweza kudokezwakwa viambishi au kwa maneno kamili. Mfano; amekaa jikoni.
Vielezi vya wakati:Vielezi vya namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokeakama maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi {po.}Mfano; alimkaribisha alipokuja.
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo. Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti.
Vitenzi vikuu (T): Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbemuhimu wa kiarifu cha sentensi. Mfano; Mtoto amekuja.
Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano , wakati, hali n.k. Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati. Mfano; Alikua anacheza, Huwa namfurahia.
Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi ambavyo hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi. Havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali.Vitenzi vishirikishi ni vya aina mbili, ambavyo nikitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi shirikishi “si” cha ukanushi.
Источник: | http://e-kayumba.blogspot.com/(1) http://e-kayumba.blogspot.com/(2) http://e-kayumba.blogspot.com/(3) http://e-kayumba.blogspot.com/(4) |