Serif
Sans serif
Monospace

bold|normal

-2|-1|N|+1|+2

Makosa katika Magazeti

Kwa usahihi mwandishi angeandika,
"Tangu niishi dunia ya wazungu nimejifunza jambo moja."
"Mwalimu Nyerere alikataa ombi hilo katika mahojiano na gazeti la Raia Mwema."
Katika maadili ya uandishi haitakiwi kutaja jina la gazeti katika masuala nyeti kwani mwandishi anaweza kushtakiwa kwa kosa la kukashifu au kuharibu jina la gazeti hilo (defamation). Hali hii pia inatumika wakati tunapoandikwa mambo nyeti yanayomhusu mtu fulani. Hatumtaji jina halisi na hivyo tunatumia jina bandia.
"Baada ya kumwona mpenzi wake Sofia akicheza na mtu mwingine walipokuwa dansini na baada majibizano mafupi alitoa bastola na kumuua mpenzi wake kwanza kabla ya kujiua mwenyewe."
Ijapokuwa tumezoea kutumia neno 'dansini' tunaweza kusema 'walipokuwa wakicheza dansi'.
Stephenjmmaina1965@yahoo.com

Mara kwa mara tunakutana na maandishi ambayo wakati mwingine yanakera. Unajiulza hivi mwandishi alipitia mfumo wa elimu ya sekondari na baadaye kusomea uandishi wa habari kwa miaka miwili? Je, kwa nini hakuona makosa haya? Jibu ni wazi. Yako matatizo mengi mojawapo ni tatizo la walimu kuwa na uwezo mdogo wa kitaaaluma. Pia vitabu havipo vyenye mada zilizotungwa hatua kwa hatua katika misingi inayotakiwa.

"Alitaka mabadiliko ya teknologia ya muundo wa meli nyingi mpya ambazo zinajengwa huku haziwekewi vifaa vya kupakuwa mizigo kuwa ni tatizo jingine."

Inatakiwa kuandika upya sentensi hii ili kuleta maana iliyokusudiwa. Kwa mfano maneno 'huku haziwekewi vifaa vya kupakuliwa' ilipaswa kuandikwa 'bila kuwekewa…" Pia neno 'teknologia lilitakiwa kuandikwa 'teknolojia'. Tatu, kupakiwa lingeandikwa 'kupakua' kwani tahajia iliyozoeleka ni pakua na siyo pakuwa. Kwa usahihi iandikwe,

"Alitaja mabadiliko ya teknolojia ya muundo wa meli nyingi mpya ambazo zinajengwa bila kuwekwa vifaa vya kupakua mizigo kuwa n tatizo jingine."

"Akizungumza jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mech Sadik alitoa tahadhari kwa wakazi na wageni wanaoingia kuhakikisha wanachukua tahadhari ili kuepuka madhara ya mafuriko."

Tatizo limejitokeza katika kutumia neno 'tahadhari' badala ya 'hadhari'. Wengi tunachanganya maneno haya hasa kwa wale ambao wamejifunza Kiswahili darasani au mitaani kama lugha ya pili. Hata walimu wetu wa Kiswahili ambao Kiswahili ni lugha yao ya pili wanashindwa kutofautisha maaneno haya. Neno tahadhari ni kitenzi wakati hadhari ni nomino. Tunachukua hadhari na wala si tahadhari. Tunasema, 'Chukua hadhari hasa kipindi hiki cha mvua ili kuepuka madhara ya mafuriko na 'Tahadhari' kabla ya hatari/athari'.

"Afrika Kusini na Malawi watashiriki ili kutafuta fursa mbalimbali za kiuchumi na kuimarisha mahusiano baina yao."

Si sahihi kusema 'mahusiano' ijapokuwa baadhi ya wanasiasa na watangazaji redioni na kwenye runinga wamelitumia sana neno hili. Sahihi ni uhusiano. Epuka pia neno 'mashirikiano' na badala yake tumia 'ushirikiano'

"CRC yapokea kesi 107 za ulevi wa pombe (Kupindikua)."

Si sahihi kutumia ufupisho katika sentensi bila kutoa ufafanuzi au maelezo ya utambulisho. Pa kuongeza nenp 'kupindukia na kuliwekea alama za mabano ni makosa kwani lilitakiwa kuongezewa taarifa zaidi. Ingewezekana kusema kuwa ni ulevi wa kupindukia au hata kutoliandika kabisa.

Mpangilio wa maneno katika sentensi kitaalamu unafahamika kama sintaksia ni taaluma muhimu kaika lugha. Angalia sentensi ifuatayo:

"Tangu asubuhi ya saa tatu hadi jioni hali ilikuwa mbaya njini hapa baada ya makunndi kadhaa ya watu, wengi wao wakiwa vijana kupambana na FFU."

Hatuandiki 'asubuhi ya saa tatu' ijapokuwa katika mazungumzo inawezekana. Sahihi ni:

"Tangu saa tatu asubuhi hadi jioni, hali ilikuwa mbaya mjini hapa baada ya makundi kadhaa ya watu, wengi wao wakiwa vijana kupambana na askari wa kupamanba na ghasia (FFU). Kifupi cha askari wa kupambana na ghasia kinaandikwa kama FFU kwa maana ya 'Field Force Unit'. Wasomaji wataelewa bila hata kuandika kwa kirefu.

"Toka niishi dunia ya Wazungu nimejifunza jambo moja."

Kutokana na mazoea waandishi hupenda kuandika 'toka' badala ya 'tangu' wanapozungumzia kipindi fulani. Maana ya toka ni kuondoka mahali na kwenda kwingine.

Iko methali isemayo," Kitokacho matumboni ki uchungu."

Maana ya tangu ni kuonesha mwanzo wa kutenda jambo. Kwa mfano 'Tangu nifike hapa hujanijali.'

Kwa usahihi mwandishi angeandika,

"Tangu niishi dunia ya wazungu nimejifunza jambo moja."

"Mwalimu Nyerere alikataa ombi hilo katika mahojiano na gazeti la Raia Mwema."

Katika maadili ya uandishi haitakiwi kutaja jina la gazeti katika masuala nyeti kwani mwandishi anaweza kushtakiwa kwa kosa la kukashifu au kuharibu jina la gazeti hilo (defamation). Hali hii pia inatumika wakati tunapoandikwa mambo nyeti yanayomhusu mtu fulani. Hatumtaji jina halisi na hivyo tunatumia jina bandia.

"Baada ya kumwona mpenzi wake Sofia akicheza na mtu mwingine walipokuwa dansini na baada majibizano mafupi alitoa bastola na kumuua mpenzi wake kwanza kabla ya kujiua mwenyewe."

Ijapokuwa tumezoea kutumia neno 'dansini ' tunaweza kusema 'walipokuwa wakicheza dansi'.

stephenjmmaina1965@yahoo.com

Источник: http://www.mwananchi.co.tz/