Wiki hii tutajadili kuhusu aina za sentensi na kufuatiwa na uchambuzi wake wiki ijayo.
Wiki iliyopita nilidokeza kuhusu mbinu za kuchanganua mofimu zilizojitokeza kwenye mzizi wa neno. Hata hivyo mwanafunzi anapaswa kufanya mazoezi kwa kadiri awezavyo ili aweze kuondokana na kero ya kufeli maswali yatokanayo na mada hiyo.
Wiki hii tutajadili kuhusu aina za sentensi na kufuatiwa na uchambuzi wake wiki ijayo. Ieleweke kwamba kwa mwanafunzi wa kidato cha nne hana budi kufanya mapitio kwa makini kwa mada zilizopita hususan aina za maneno, vishazi ambazo ni mojawapo ya maeneo yanayoweza kumfanikisha mwanafunzi kumudu vyema kubaini na kuchanganua aina za sentensi.
Ni vyema kubaini aina ya sentensi iliyojitokeza pia kujua kiima na kiarifu ama kikundi cha maneno kilichojitokeza kwa kila upande. Hii itakusaidia kubainisha aina za maneno kwa kila upande au kikundi kilichojitokeza.
Baada ya kuelewa eneo hilo mwanafunzi anaweza kuchagua mkabala ili kufanya uchanganuzi wa sentensi. Miongoni mwa mikabala unaoweza kutumia ni matawi, maneno na mshale. Mathalan kuna aina tatu za sentensi nazo ni sahili, ambatano na changamano. Wataalamu wengine huelezea pia uwapo wa aina ya sentensi shurutia.
Tunaweza kubaini sentensi sahili kutokana na kuwapo muundo ufuatao.
Sentensi sahili kutokana na kikundi tenzi pekee:
Pia muundo wa Kikundi Nomino + Kikundi Tenzi
Sentensi ambatano ni sentensi zenye zaidi ya kishazi huru kimoja na huwakilisha mawazo mawili au zaidi. Aghalabu sentensi hizi hutumia viunganishi (U) au alama za uakifishaji kama vile mkato (,) na nuktamkato (;) ili kubainisha wazo moja. Tuangalie mfano katika kuunganisha sentensi mbili:
Pia tunapata sentensi: Kaka yangu amerudi nyumbani na kulala.
Sentensi Changamano ni sentensi zinazoundwa kwa kuunganisha kishazi huru pamoja na kishazi tegemezi au sentensi mbili kwa kutumia o- rejeshi ili kuleta zaidi ya wazo moja.
Jinsi ya kupata sentensi changamano kwa kuunganisha sentensi:
Mfano mwingine ni: Yeye ni jambazi. Alipigwa jana jioni. Hivyo tunapata sentensi ifuatayo: Yeye ndiye jambazi aliyepigwa jana jioni.
Mwanafunzi hapaswi kukariri mfuatano wowote wa maneno isipokuwa ni vyema mwanafunzi akafahamu kanuni ya mfuatano wa maneno. Kwa kufahamu aina mbalimbali za maneno na mazingira yanapojitokeza itamwezesha mwanafunzi kutobabaika na aina yoyote ya sentensi ambayo atakutana nayo.
Hivyo basi ili kutofautisha sentensi ambatano na changamano kwa urahisi, sentensi changamano hutumia o-rejeshi ( ambacho, ambaye, niliye , nililo- n.k).
Zoezi: Bainisha na ainisha sentensi zifuatazo:
Mwandishi ni mtaalamu wa Kiswahili.
Источник: http://www.mwananchi.co.tz/